×

Rais Samia Afanya Uteuzi wa Makamishna Wa Jeshi La Polisi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Kombo Khamis Kombo kuwa Kamishna wa Polisi huku akimteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar ana anachukua nafasi ya CP. Hamad Khamis Hamad ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia pia amempandisha Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Tatu Rashid Jumbe kuwa Kamishna wa Polisi na kumteua kuwa Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu katika Jeshi la Polisi akichukua nafasi ya CP. Suzan Kaganda ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

MSIGWA ATAJA CHANZO cha UGOMVI CHADEMA – “KUNA BWANA MKUBWA AMEJIMILIKISHA CHAMA – AMEPANGA TIMU”…

Leave a Comment