
Klabu ya Yanga leo Desemba 11, 2024 imemtambulisha aliyekuwa beki wa pembeni wa Simba, Israel Patrick Mwenda kama mchezaji mpya klabuni hapo akitokea Singida Black Stars yenye maskani yake CCM Liti, Singida.
Mwenda ambaye anachezea nafasi ya beki wa kulia pia anamudu kucheza kama beki wa kushoto anatarajiwa kuja kutibu matatizo yote kwenye nafasi ya beki wa kulia na kushoto na anakuja kuwa changamoto Kouassi Attohoula Yao, Shadrack Boka, Nickson Kibabage na Kibwana Shomari ambao wameonekana kuandamwa na majeraha sambamba na viwango kushuka.