
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema Dira mpya ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 itazingatia misingi sita muhimu inayopaswa kulindwa na kila mmoja wakiwemo Wanasiasa na vyama vya siasa.
Ameitaja misingi hiyo kuwa ni umoja, utu, uhuru na haki, demokrasia, ulinzi wa maliasili na rasilimali pamoja na ulinzi wa utamaduni na maadili ya taifa.
Waziri Kitila Mkumbo amebainisha hayo leo Jumamosi Desemba 14, 2024 wakati wa mkutano wa vyama vya siasa na Tume ya Mipango katika kuhakiki Rasimu ya kwanza ya Kwanza ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, kazi ambayo itakutanisha kamati hiyo na makundi mbalimbali ya kijamii ili kuhakiki ikiwa maoni yao yamezingatiwa katika rasimu ya Dira 2050.
Amesema dira hiyo inalenga kujenga taifa jumuishi, lenye haki, ustawi na linalojitegemea.