The House of Social Media
gunners X

Polisi: Daisle Simion Ulomi Alipata Ajali ya Bodaboda, Akafariki – Video

0

JESHI la Polisi Tanzania limesema kuwa baada ya kufanya ufuatiliaji kwa kushirikiana na ndugu wa mfanyabiashara, Daisle Simion Ulomi aliyedaiwa kupotea mnamo Desemba 11, 2024 imebainika kuwa alipata ajali mbaya ya pikipiki aliyokuwa akiitumia na kupelekwa katika kituo cha afya cha Makuburi External Ubungo na Wasamaria wema akiwa hajitambui.

Taarifa ya Desemba 16, 2024 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, SACP Muliro J Muliro imeeleza kuwa Ulomi alihamishiwa katika hospitali ya Mwananyamala ambako ilibainika kuwa tayari alikuwa amefariki na maiti yake kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mwananyamala kama mtu asiyefahamika akisubiri kutambuliwa na ndugu.

“Ndugu tayari wameutambua mwili huo ukiwa na majeraha maeneo mbalimbali ya mwili. Aidha, Pikipiki aliyopata nayo ajali pia imepatikana ikiwa imeharibika. Uchunguzi zaidi wa ajali hiyo unaendelea na taarifa zaidi itatolewa.”——imesema taarifa hiyo

Mnamo tarehe 11 Desemba 2024, Jeshi la Polisi lilipata taarifa ya kupotea kwa Ulomi na ndugu hawakuwa wanampata kwenye mawasiliano ya simu baada ya yeye kuondoka ofisini kwake Sinza akitumia pikipiki namba MC 415 DQC aliyokuwa akiendesha mwenyewe na kudai anaelekea Temeke kufuatilia makontena yake ya biashara.

Leave A Reply