
Usiku wa kuamkia leo Disemba 20, 2024 matokeo ya uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa Kanda ya kaskazini yametangazwa ambapo Wakili Samwel Welwel ameshinda kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda akichukua nafasi ya Godbless Lema.
Welwel ameshinda kwa kura 51 sawa na asilimia 51.5%, huku mpinzani wake Michael Kilawila akipata kura 48 sawa na asilimia 48.5%. Wapiga kura walikuwa 100 na hakuna kura iliyoharibika.
Uchaguzi huo ulilazimika kufanyika mara mbili kutokana na uchaguzi wa kwanza kura kutokutosha. Utaratibu wa CHADEMA unasema mshindi kwa nafasi ya Uenyekiti anatakiwa kuwa na kura kuanzia asilimia 50 na kuendelea.
Matokeo ya kwanza ambapo wagombea walikuwa watatu Anthony Mallya alipata 12 sawa na asilimia 12%, Samwel Welwel alipata kura 42 sawa na asilimia 42% huku Michael Kilawila akipata kura 46 sawa na asilimia 46%.