
Habari hii ni ya kusikitisha mno! Inamhusu mtoto Grayson Kanyenye mwenye umri wa miaka sita (6), ambaye ni mtoto wa mmiliki wa saluni ya Jojo Ladies Point iliyopo jijini Dodoma, Zaituni Shabani.
Mtoto Grayson, aliyekuwa akiishi na familia yake katika maeneo ya Majengo Mapya – Area D, jijini Dodoma, ameuawa kinyama kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na watu wasiojulikana.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limethibitisha kupokea taarifa hiyo na limesema kuwa taarifa rasmi kuhusu kifo hicho itatolewa baadaye.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, RPC George Katabazi, ameieleza kuwa Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi wa kifo hicho.
Mtoto Grayson alikutwa ameuawa kwa kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali, hasa maeneo ya kichwani, na watu wasiojulikana.
Mtoto Grayson atazikwa leo katika makaburi ya Kilimo Kwanza, baada ya ibada itakayofanyika kuanzia saa sita mchana nyumbani kwao.