
Msanii wa muziki maarufu nchini Tanzania, Amber Lulu, ameweka wazi hisia zake kuhusu tofauti zinazodaiwa kuwepo kati yake na wasanii wenzake wa kike, Gigy Money na Nai.
Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni katika usiku wa Rose Ndauka, Amber Lulu alisema hana tatizo binafsi na Gigy Money wala Nai, akiongeza kuwa changamoto zilizopo ni za kawaida katika uhusiano wa kibinadamu, hasa katika tasnia ya burudani ambayo mara nyingi huzongwa na ushindani mkubwa.