
Kocha wa klabu ya JKT Tanzania, Ahmad Ally ambaye amekabidhiwa mikoba ya kukinoa Kikosi cha Kilimanjaro Stars kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo ya Kombe la Mapinduzi 2025 ametaja kikosi kitakachoingia kambini kwa ajili ya mashindano hayo.
Mashindano ya Mapinduzi Cup 2025 yatafanyika Pemba msimu huu zikihusika timu za Taifa. Kikosi hicho hakijahusisha wachezaji wa Simba na Yanga kwakuwa watakuwa kwenye majukumu ya mashindano ya CAFCL na Kombe la Shirikisho.
