×

Rais Ruto Akiri Mapungufu Ya Vikosi Vya Usalama

Rais wa Kenya, William Ruto, jana Jumanne amekiri ukiukaji unaofanywa na vikosi vya usalama vya Kenya, kufuatia maandamano dhidi ya wimbi la karibuni la tuhuma za utekaji ambalo limezua ghadhabu kwa wananchi nchini humo.

Katiba hotuba yake ya mwaka mpya Rais Ruto amesema haiwezi kukanushwa kuwa kumekuwa na vitendo vya kupita kiasi na visivyo vya kisheria vya maafisa wa idara ya usalama.

Vikosi vya usalama katika taifa hilo la Afrika Mashariki vimeshutumiwa kwa kuwashikilia watu kadhaa kinyume cha sheria tangu maandamano yaliyoongozwa na vijana dhidi ya serikali mwezi Juni na Julai kukandamizwa vikali.

Jumatatu, polisi waliwashikilia kwa nguvu mamia ya waandamanaji na kutumia gesi ya kutoa machozi katika maandamano ya amani ya kutaka kuachiliwa kwa wale ambao waliotoweka.
Wiki iliyopita, rais anayekabiliwa na mzozo aliahidi kukomesha utekaji.

Stori na Elvan Stambuli | GPL

MKUU wa MKOA wa MWANZA – SAID MTANDA AITISHA MAOMBI kwa AJILI ya NCHI na RAIS SAMIA…

Leave a Comment