
Alute Munghwai, kaka wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu ameeleza kuwa ni muhimu kurekebisha katiba ya chama hicho baada ya uchaguzi wa ndani ya chama.
Ameongeza kuwa kiongozi atakayechaguliwa atapaswa kuwa na jukumu la kurekebisha katiba ya chama chao ili kuhakikisha mafanikio ya chama.
Pia amesema kama yapo mambo ambayo ndugu yake hakutakiwa kuyazungumza hadharani kuhusu chama, lazima atahojiwa na chama chake na kusisitiza kuwa hata Mbowe yapo mambo aliyozungumza ambayo si sahihi.
Alute ambaye ni mwanachama wa CCM, amesema Mwenyekiti Freeman Mbowe, naye anajitapa kuwa ni tajiri na kuwaita wengine kuwa ni wabangaizaji na hawawezi kugombea uenyekiti wa Chadema, jambo ambalo amesema ni kinyume na katiba yao.