×

Rais Samia na Mwinyi Kugombea Urais 2025, Azimio Kuwasilishwa – Video

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amesema kama wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakitaka wanaweza kuamua kwamba Rais Samia Suluhu Hassan awe mgombea pekee wa nafasi ya urais ndani ya chama sambamba na Dk. Hussein Mwinyi kwa upande wa Zanzibar.

Kauli hiyo ya Kikwete ikapokelewa kwa shangwe kubwa kutoka kwa wajumbe ambao walianza kushangilia huku wakilitaja jina la Rais Samia.

Akaongeza kuwa kama wajumbe wote wamekubaliana, lazima lipitishwe azimio ambalo litarasimisha na kumfanya Rais Samia kuwa mgombea pekee sambamba na Dk. Mwinyi kwa upande wa Zanzibar.

Leave a Comment