Donald Trump aiondoa Marekani kwenye Mkataba wa Paris

Rais Donald Trump ameanza kutekeleza baadhi ya ahadi alizoahidi wakati wa kampeni, ambapo ametia saini maagizo kadhaa, kama vile makubaliano ya hali ya hewa ya Paris ya 2015.
Rais Donald Trump ameiondoa nchi yake ambayo ndiyo mtoaji mkubwa wa gesi chafuzi duniani, kutoka kwenye juhudi za ulimwengu za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi kwa mara ya pili katika kipindi cha mwongo mmoja.
Trump ametia saini amri hiyo ya kuiondoa Marekani kwenye mkataba huo mbele ya wafuasi wake waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Capital One Arena mjini Washington.
“Unafikiri Biden angeweza kufanya hivi? Sidhani,” Trump aliwaambia wafuasi wake waliokuwa wakimshangilia huku akiwarushia kalamu alizotumia kusaini maagizo ya rais Joe Baden.
Hatua hiyo inaiweka Marekani pamoja na Iran, Libya na Yemen kama nchi pekee duniani ambazo haziko kwenye mkataba huo wa Paris wa mwaka 2015.
Rais Trump ambaye ni rais wa 47 wa Marekani amekuwa akipinga mabadiliko ya tabia nchi na kudai ni hekaya tu. Aliiondoa Marekani kutoka kwenye mkataba wa Paris alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza, ingawa mchakato huo ulichukua miaka lakini Biden alisaini mara moja amri ya kuirejesha Marekani alipochukua uongozi.
Stori: Elvan Stambuli | GPL

