×

Daraja La Kigongo-Busisi Lafikia Asilimia 96.3, Kukamilika Februari 2025

UJENZI wa daraja la kimkakati la Kigongo Busisi mkoani Mwanza unatarajiwa kukamilika mwezi ujao huku likitarajiwa kubadili hali ya kimaisha na mwonekano wa eneo la Kanda ya Ziwa.

Akizungumza katika daraja hilo jana, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 96 hivi sasa na kama mambo yatakwenda kama yalivyo, utafikia asilimia 100 na kukamilika kabisa kufikia mwishoni mwa mwezi ujao.

Alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alisema alikuta ujenzi wa daraja hilo ukiwa umefikia kiasi cha asilimia 25 tu mwaka 2021 na sasa ametumia zaidi ya shilingi bilioni 611 kufika lilipo sasa.

Daraja hilo linatarajiwa kurahisisha usafiri katika eneo zima la kanda ya ziwa kwa kupunguza muda wa usafiri kuvuka kutoka eneo hilo kutoka saa mbili za sasa hadi dakika tano baada ya kukamilika kwa daraja.

Leave a Comment