
Mkazi wa Kijiji cha Chambo, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Zaharani Patrombeyu (44), ambaye alikuwa mkuu wa Shule ya Sekondari Chambo, amefariki dunia baada ya kunywa kitu kinachodhaniwa kuwa sumu nyumbani kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza kuwa Zaharani alikunywa sumu hiyo Januari 29 majira ya saa tano. Alipozidiwa, alipelekwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama kwa matibabu, lakini alifariki dunia Januari 30.
Kamanda Magomi amesema kuwa chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa na ametoa wito kwa wananchi wa Shinyanga kuepuka kuchukua sheria mkononi, badala yake watafute msaada kwa viongozi wa dini au wataalamu wa saikolojia wanapokabiliwa na matatizo.