
Msanii wa maigizo nchini, Amina Vikoba, amefunguka kuhusu siri ya kuwa na muonekano mzuri licha ya kutimiza miaka 40. Akizungumza katika sherehe ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika Tabata Hoteli, jijini Dar es Salaam, Amina alisema kuwa uzuri wake unatokana na mtindo mzuri wa maisha, utunzaji wa ngozi, na kuepuka msongo wa mawazo.
Amina, ambaye amekuwa kivutio kwa mashabiki wake kwa muda mrefu, aliwataka vijana wa kizazi kipya, hasa wale wa miaka ya 2000, kuwa makini na maamuzi yao, hususan wanapopata watu wanaowatongoza. “Sio kila mtu akikuambia jambo unakubali tu kwa ‘ndio.’ Jifunzeni kusema hapana pale inapobidi,” alisema Amina.