×

Ofisi Ya Ras Mkoa Wa Arusha Yaipongeza Halmashauri Ya Wilaya Ya Longido Kwa Usimamizi Mzuri Wa Ukusanyaji Wa Mapato Na Miradi Ya Maendeleo

Longido, Februari 7, 2025 – Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido umepongezwa kwa usimamizi mzuri wa mapato, utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pamoja na maandalizi bora ya taarifa za halmashauri.

Pongezi hizo zimetolewa na Ramadhani Madereka Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) kwa seksheni ya Utawala ,Usimamizi na Ufuatiliaji (MMI) Mkoa wa Arusha wakati wa mkutano wa kawaida wa baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri, ambapo alieleza kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na uongozi wa halmashauri katika kuhakikisha rasilimali zinatumika ipasavyo kwa maendeleo ya wananchi.

“Nimeona kazi nzuri inayofanyika katika ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa miradi, na hata namna taarifa zinavyoandaliwa kwa uwazi na umakini,kweli Longido hii siyo ile ya zamani mmepiga hatua kwa kiasi kikubwa sana . Haya ni mafanikio yanayostahili pongezi,” alisema Bw. Madereka

Aidha, alisisitiza kuwa fedha zinazokusanywa zinapaswa kutumika kwa uangalifu na kwa manufaa ya Wilaya ya Longido, akitoa wito kwa viongozi wa halmashauri kuendelea kusimamia matumizi bora ya rasilimali ili kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa halmashauri, madiwani, na watendaji wa idara mbalimbali, ambapo masuala ya maendeleo ya wilaya yaliendelea kujadiliwa kwa kina.

JAJI MWAMBEGELE AWAPA MAELEKEZO VYAMA vya SIASA -“HAKIKISHA MAWAKALA WANASIMAMIA UBORESHAJI DAFTARI”