×

Mtifuano wa Fainali ya Jafo Cup Ilikuwa Balaa

Fainali ya Jafo Cup iliyopigwa jana Jumamosi katika  Uwanja wa Kijiji cha Maneromango  mtifuano wake ulikuwa ni balaa kwa jinsi burudani ilivyokuwa ya kuvutia na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa mashabiki wa burudani.
Mtifuano ulianzia kwa kumsaka mshindi wa tatu katika ya timu ya Chole na Mzenga ambapo Mzenga ndiyo waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Baada ya hapo ndipo mtifuano wa fainali ya kumsaka bingwa wa mashindano hayo kati ya Maneromango na Kisarawe ulianza huku kila timu ikionesha upinzani mkali na kuibukia na ushindi lakini ilibidi uingie hatua ya mikwaju ya penati baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1.
Mikwaju hiyo ndiyo iliyotoa uamuzi wa Maneromango kushinda kwa mikwaju 5-4 na kuibua shangwe la aina yake kwenye viwanja hivyo.
Akizungumza baada mashindano hayo, Mbunge wa Jimbo la Kisarawe na Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye aliyekuwa mgeni rasmi na ndiye muandaaji wa mashindano hayo aliwapongeza washiriki wote wa mashindano hayo pamoja na umati mkubwa uliofika kushuhudia mashindano hayo.     HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN/ GLOBAL PUBLISHERS