×

Watu 80 Wanusurika kifo Katika Ajali ya Ndege Canada

Takribani watu 18 wamejeruhiwa baada ya Ndege ya Ndege ya Delta namba 4819 iliyokuwa ikitokea Minneapolis Marekani kwenda Toronto, Canada ikiwa na Abiria 80 kupinduka na kuwaka moto majira ya saa 8:15 usiku kwa saa za huko baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Toronto Nchini Canada.

Abiria wote wameondolewa kwenye Ndege hiyo huku majeruhi hao 18 wakitibiwa majeraha kufuatia ajali hiyo, wakiwemo watatu waliojeruhiwa vibaya na kupelekwa katika hospitali za eneo hilo.

Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa ni upepo mkali ulioripotiwa katika Jiji la Toronto kwa siku nzima ya Jumatatu uliovuma kwa kasi takriban 20-30 mph ambao ulifikia 40 mph

JEMIMAH ALILIA TALAKA na KUACHA MALI za MABILIONI -”KUUAWA DKK 1-SIRI YANGU-KITU KIZITO JIFUNZENI”