×

Eric Shigongo: Watanzania Tembeeni Vifua Mbele, Nchi Yenu Ni Tajiri – Video

Mbunge wa Buchosa na Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo

Baada ya kurejea kutoka nchini Marekani ambako alikuwa kwenye ziara ya kikazi, Mbunge wa Buchosa na Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo, amezungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi, Februari 22, 2025, katika Ofisi za Global Group, Sinza Mori, jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo uliorushwa moja kwa moja kupitia Global TV, Shigongo alisisitiza kuwa Watanzania hawapaswi kuwa wanyonge, bali wanapaswa kutembea vifua mbele kwa fahari, kwani Tanzania ni nchi tajiri yenye rasilimali nyingi.

Aidha, alitoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuhakikisha Tanzania inajitegemea kiuchumi kwa kutumia rasilimali zake. Alisema kuwa mkakati wa kujitegemea utaifanya nchi kuendelea kwa kasi na kuwapatia wananchi fursa nyingi za maendeleo.

Katika hotuba yake, Shigongo alihimiza uzalendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania, akiwataka waamini katika uwezo wao wa kuleta mabadiliko chanya kupitia bidii na ubunifu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.