
Kampuni ya ALAF Limited imeahidi kuendelea kuwawezesha wafanyakazi wa kampuni hiyo kuimarisha afya ya mwili na akili ili kuzidisha ufanisi wao katika kazi.
Hayo yameelezwa na Meneja Rasilimali Watu wa kampuni ya ALAF Jumbe Onjero wakati akitoa taarifa kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk Doto Biteko alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye Maonyesho ya The People’s Expo.
Maonyesho hayo yalikuwa ni sehemu ya matukio yanayohusiana na mbio za kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon yaliyofanyika Jumapili Februari 23, 2025, katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) mjini Moshi mjini, mkoani Kilimanjaro.
Alisema walidhamini zaidi ya washiriki 50 katika mbio za mwaka huu na kwamba ushiriki wao umekuwa jambo zuri na la kukumbukwa, amapo alisema wafanyakazi wa kampuni hiyo wlaishiriki katika vipnngele vyote vya mbio hizo ambavyo ni kilomita 42.2 za Kilimanjaro Premium Lager, mbio za kilomita 21.1 maarufu kama YAS half marathon na mbio za kujifurahisha za kilomita 5 zinazodhaminiwa na CRDB Bank.
“Tutaendelea kuunga mkono mbio hizi kwa lengo la kuinua sekta ya michezo sambamba na kuhakikisha wafanyakazi wetu wanafanya mazoezi yatakyoimarisha afya zao kupitia mbio za Kilimanjaro International Marathon”, alisema.
Alisema hivi karibuni ALAF ilizindua klabu yake ya jogging inayojumuisha wafanyakazi kutoka vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo ambapo wafanyakazi wataendelea kufanya mazoezi kwa ajili ya kushiriki mbio mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon.
Kuhusu Maonesho yanayoendana na mbio hizo, alisema hii ni mara ya kwanza kwa ALAF kushiriki katika hafla hiyo inayokutanisha zaidi ya watu 20,000 kwa wakati mmoja.
“Mbio hizi pamoja na maonyesho haya ni moja ya matukio makubwa nchini Tanzania na kama kampuni iliyojizatiti kuboresha maisha ya watu kupitia bidhaa na huduma zake kwa ujumla, tulipata fursa ya kuwasiliana moja kwa moja na wateja wetu na kujibu maswali kuhusiana na hudma zetu waliyowasilisha,” alisema.
Aidha alibainisha kuwa maonyesho hayo yalikuwa ni fursa nzuri kwa kampuni hiyo kuwafahamisha wateja wake ya mwishoni mwa mwaka jana, ALAF imeanza uzalishaji wa mabati ya rangi kupitia mtambo wake mpya wa mabati ya rangi.
Kampuni ya ALAF Limited (ALAF) ni kampuni inayoongoza kwa utengenezaji wa vifaa vya chuma vyenye ubora wa hali ya juu ambavyo ni maalum kwa ajili kuezekea paa za nyumba.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 1960, ALAF imeendelea kutoa mchango mkubwa katika sekta ya ujenzi hapa nchini.
Shughuli za ALAF hazihusiani na uzalishaji wa vifaa vya chuma za kuezekea tu bali pia ianjihusisha na uzalishaji wa koili za chuma zilionakshiwa kwa rangi kwa ajili ya matumizi mablimbali kwenye sekta ya ujenzi pamoja na mirija ya chuma na mabomba kwa ajili ya matumizi mbalimbali.