×

YANGA VS SIMBA… Rekodi zinaibeba Yanga

KWENYE misimu 11 ya hivi karibuni ambapo wababe Yanga na Simba wamekutana, Yanga inashikilia rekodi ya kupindua meza kibabe, kwenye jumla ya mechi 23.

 

Katika mechi hizo, Yanga imeshinda sita, Simba saba na sare kumi. Rekodi zinaonyesha kuwa, ni mechi nane tu timu ilitoka nyuma na kupindua matokeo kwa kuweka mzani sawa na kugawana pointi.

 

Yanga inaongoza kupindua matokeo ikiwa imetoka nyuma mara tano, huku Simba ikitokea nyuma mara tatu. Tazama hapa ilivyokuwa upande wa Yanga: Msimu wa 2008/2009, Aprili 19, matokeo yalikuwa sare ya 2-2, Simba ilianza kupata bao dakika ya 23 kupitia kwa Ramadhan Chombo, likasawazishwa na Ben Mwalala dakika ya 48. Haruna Moshi Boban akaongeza bao la pili kwa Simba dakika ya 62, Jerry Tegete akasawazisha dakika ya 90.

Oktoba 3 katika msimu wa 2012/13, mchezo uliisha kwa sare ya 1-1, Simba ilianza kufunga dakika ya tatu kupitia kwa Amri Kiemba, Yanga ikarudisha dakika ya 65 kwa bao la Said Bahanuzi.

 

Msimu wa 2013/14. Aprili 19, Yanga 1-1 Simba. Simba ilianza kufunga dakika ya 76 kupitia kwa Haruna Chanongo, Simon Msuva akasawazisha dakika ya 86. Msimu wa 2017/18. Mechi ilichezwa Oktoba 28, matokeo yakiwa 1-1, Simba ilianza tena kufunga dakika ya 58 kupitia kwa Shiza Kichuya, Obrey Chirwa akasawazisha dakika ya 60. Msimu wa 2019/20, Januari 4, 2020.

 

Simba 2-2 Yanga. Simba ilianza kufunga kupitia kwa Meddie Kagere dakika ya 42 na Deo Kanda akaongeza la pili dakika ya 46. Yanga ilipindua matokeo kupitia kwa Mapinduzi Balama dakika ya 49 na beki wa Simba, Mohamed Hussein akajifunga dakika ya 53. Upande wa Simba, mambo ya kupindua matokeo mbele ya Yanga yalikuwa hivi: Msimu wa 2010/11, Machi 5 kwenye sare ya 1-1, Yanga ilianza kufunga dakika ya 59 kupitia kwa Stephan Mwasyika, lilipinduliwa na Mussa Mgosi dakika ya 73. 2013/14, Oktoba 20, Yanga 3-3 Simba, Yanga ilianza kufunga mabao kipindi cha kwanza kupitia kwa Mrisho Ngassa dakika ya 15, Hamis Kiiza (dk 35 na 45). Simba ilipindua kupitia kwa Betram Mwombeki dakika ya 54, Joseph Owino (dk 58) na Gilbert Kaze (dk 85). Msimu wa 2016/17, Oktoba Mosi, Simba 1-1 Yanga. Yanga ilianza kufunga kupitia kwa    Amiss Tambwe dakika ya 26, lilipinduliwa na Shiza Kichuya dakika ya 8.

YANGA Watengewa MIL 200 Kuwafunga SIMBA Tar 08, NUGAZ Afunguka WALIVYOJIPANGA…


 

Leave a Comment