×

Nafasi za Kazi 10 Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Mwisho wa maombi Machi 6, 2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kuomba nafasi ya kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

1.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 10
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; na
vi. Kufanya Usafi wa gari.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 06 Machi, 2025

BONYEZA HAPA KUSOMA >>>TANGAZO LA NAFASI DEREVA DARAJA LA II WILAYA YA ILEJE