×

Sakina Lyoka Kuhakikisha Aziz Ki Na Hamisa Mobetto Wanasafiri Dubai Kwa Fungate

Kampuni ya Bicco Express imemtangaza rasmi mtangazaji maarufu nchini, Sakina Lyoka, kuwa Balozi wao kuelekea Msimu wa Mwezi wa Ramadhani.

Bicco Express, inayojulikana kwa huduma zake za uhakika katika ukataji wa tiketi za ndege kwa safari za kimataifa na za ndani ya Tanzania, imeeleza kuwa Sakina ni chaguo sahihi kutokana na ushawishi wake katika jamii.

Baada ya kutangazwa kama Balozi, Sakina Lyoka alieleza kuwa atahakikisha wapenzi Aziz Ki na Hamisa Mobetto wanapata fungate bora Dubai kwa kuwakatia tiketi kupitia Bicco Express.

Alisema kuwa huduma za kampuni hiyo zinawapa abiria safari za haraka na zisizo na usumbufu, akisisitiza kuwa atahakikisha wanapata tiketi zao kwa wakati na kwa urahisi.

Pamoja na kuwakatia tiketi Aziz Ki na Hamisa Mobetto, Bicco Express pia imemzawadia Sakina Lyoka safari ya kifahari kwenda Dubai kama sehemu ya kuthamini mchango wake kama Balozi wa kampuni hiyo.

 

SAKINA LYOKA ALIVYOTANGAZWA KUWA BALOZI