
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amegawa boti (Awamu ya pili) kubwa 35 za kisasa na vifaa vyake kwa wavuvi wa Pangani jijini Tanga, wizara imepokea shilingi bilioni 11.5 na kununua boti 120 kati ya boti 120 zilizotolewa nchi nzima, mkoa wa Tanga umepata boti 35 ni sawa na asilimia 29.
Pamoja na Rais kugawa boti hizo, wavuvi wamepongeza jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakopesha boti ambazo ni za kisasa na imara zaidi za mwanzo walizokuwa wanatumia.
Pia Rais Samia aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la Mto Pangani na Barabara ya Bagamoyo (Makurunge) – Saadani na Tanga – Pangani.
