×

Uchambuzi wa Asasi za Kiraia Kuhusu Ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uchaguzi 2025

Asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu tuna jukumu muhimu katika jamii la kulinda na kutetea haki za binadamu, pamoja na kufuatilia masuala ya uwajibikaji na utawala bora.

Kufuatia Tume iliyoundwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuchunguza matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 na kuwasilisha taarifa yake hadharani tarehe 23 Aprili 2026, tumeona kuwa tuna wajibu wa kufanya uchambuzi wa awali wa taarifa hiyo na kutoa maoni yetu kwa umma.

Taarifa hii fupi inalenga kubainisha baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika ripoti hiyo pamoja na kutoa mapendekezo ya hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa ili kuboresha mchakato wa uwajibikaji na uimarishaji wa haki za binadamu.

Pamoja na kwamba tangu awali tulieleza kutoridhishwa kwetu na muundo wa Tume hiyo, hasa kwa kutokuwashirikisha kikamilifu wadau wote muhimu wakiwemo wataalamu huru wa kimataifa wenye uzoefu katika uchunguzi wa aina hii ya matukio, bado tunaona ni muhimu kutoa uchambuzi wa kina wa taarifa hiyo, kubainisha mapungufu yake, na kutoa mapendekezo yetu kwa maslahi ya haki, ukweli na uwazi kwa jamii.

Leave a Comment