×

Kijana wa Rais Putin Aibuka Mshindi wa Kwanza wa Mashindano ya Qurani ya Mabara – Video

 

Kijana kutoka Urusi, Aiemiddin Farkhudinov mwenye umri wa miaka 23 amekuwa mshindi wa kwanza wa Mashindano ya 25 ya Mabara yote yaliyofanyika leo Machi 16, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwa ushindi huo, kijana huyo kutoka kwa Rais Putin anaondoka na kitita cha cha Dola za Marekani 11,308.47 (shilingi milioni 30) na Medali ya dhahabu yenye thamani ya shilingi 2,800,000.

 

Mshindi wa pili ni kijana kutoka Libya, Abdulmuhaimin Mohamed Jumah (24) aliyeondoka na Dola 7,450 (shilingi milioni 20,040,000) huku ushindi wa tatu ukienda Misri kwa kijana Eslam Mahmoud Ahmed (25) aliyeondoka shilingi 11,834,000

Nafasi ya nne imekwenda kwa Saalih Mohamed Rahim (21) kutoka Guyana (Amerika Kusini) ambaye ameondoka na takribani Dola 3,000 (shilingi milioni 8) na Mtanzania Bara, Kassim Ayoub Salim (22) akiondoka na shilingi 5,380,000.