×

CHADEMA Yaitwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kujadili kauli ‘No reform no election’

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeitwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya majadiliano.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Brenda Rupia, ajenda kuu ya kuitwa kwa chama hicho ni kujadili kauli mbiu ya ‘No reform no election’.