×

Mama Aangua Kilio Hadharani, Nyumba Yake Yauzwa Kwa Mnada Kulipa Deni Alilokopa La Milioni 30 Benki – Video

Mwanamama Asha Ramadhan, Mkazi wa Kimara Golan jijini Dar es Salaam

Mwanamama Asha Ramadhan, Mkazi wa Kimara Golan jijini Dar es Salaam, amemlilia Rais Samia Suluhu Hassan amsaidie kufuatia nyumba aliyokuwa akiishi na wanaye, kupigwa mnada kutokana na deni alilokopa.

Mwanamama huyo ameeleza kuwa alikopa kiasi cha shilingi milioni 30 na kutakiwa kulipa shilingi milioni 57 ambapo wakati wa marejesho, akiwa amelipa kati ya shilingi milioni 14 hadi shilingi milioni 15, alipatwa na ugonjwa wa kupooza na kusababisha ashindwe kufanya chochote.

Licha ya kuwasiliana na taasisi iliyomkopesha mara kadhaa kuhusu ugonjwa wake, hakupata msaada wowote mpaka alipokuja kutolewa ndani ya nyumba hiyo na kutupiwa vitu vyake nje.