
Mkaguzi kata ya Kisangura Wilaya Serengeti Mkoa wa Mara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP) Genuine Kimario amepokea shukrani kutoka kwa mwananchi wa kata yake Emmanuel Bhoke Jackson baada ya kufanikisha huduma za awali katika hospitali ya Kanda Bugando iliyopo Jijini Mwanza.
kutokana na changamoto aliyokuwa iliyokuwa ikimkabili kwa kipindi kirefu huku mwananchi huyo akiomba msaada zaidi ili kukamilisha matibabu yake ambayo ni zaidi ya laki saba.

Akipokea shukran hizo hizo mkaguzi wa kata hiyo ameendelea kuwaomba wananchi wote kumsaidia mwananchi huyo ili alejee katika hali yake ya kawaida na kuemdelea na shughuli zake katika ujenzi wa Taifa.
Mkaguzi Kimario ameongeza kuwa mwananchi huyo bado yupo Jijini Mwananza na bado anahitaji msaada Mkubwa wa kifedha ili akamilishe matibabu yake.
Vilevile amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana nae katika eneo la Kisangura ambalo anahudumu kuhakikisha wananchi wote wanaofika katika kata hiyo wanafurahia utulivu na amani wa kata hiyo.