×

Mwandishi mkongwe Afrika, Shaka Ssali Afariki dunia

Mwandishi wa habari mkongwe Afrika, Shaka Ssali, mzaliwa wa Kabale, Uganda aliyekuwa akifanya kazi kwa muda mrefu katika Shirika la Habari la Voice of America kabla ya kustaafu, amefariki dunia.

Gazeti la Monitor la Uganda, limechapisha habari za kifo cha Shaka likieleza kuwa zimethibitishwa na Shirika la Habari la VOA alikokuwa anafanyia kazi.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Shaka amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 71, leo Alhamisi, Machi 27, 2025 Virginia nchini Marekani.

Enzi za uhai wake, Shaka alijipatia umaarufu mkubwa kupitia Kipindi cha Straight Talk Africa kilichokuwa kikirushwa na VOA.
Taarifa zaidi zitakujia.