×

CHADEMA Waitisha kikao maalum na watia nia wa nafasi za ubunge

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuitisha kikao maalum na watia nia wa nafasi za ubunge kupitia chama hicho. Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika tarehe 3 Aprili 2025 katika ofisi za makao makuu ya chama, Mikocheni, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia Machi 27, 2025, kikao hicho ni sehemu ya mikakati ya chama ya kuendelea kushirikiana na wadau wa uchaguzi, demokrasia, na ustawi wa chama, huku kikiendelea kusisitiza msimamo wake wa “No Reforms, No Election”.

CHADEMA imesisitiza kuwa taarifa zaidi kuhusu maazimio ya kikao hicho zitatolewa baada ya mkutano huo kufanyika.