
Rais Vladimir Putin amependekeza kuwa Ukraine inapaswa kuwekwa chini ya udhibiti wa Umoja wa Mataifa (UN) kwa muda ili kuchagua kile alichokiita serikali yenye uwezo zaidi.
Ni jaribio la hivi punde la rais wa Urusi kupinga uhalali wa serikali ya Valensiky. Ukraine nayo ilimshutumu Putin kwa kupendekeza mawazo ya ukichaa ili kuchelewesha harakati zaidi kuelekea makubaliano ya amani – ambayo yanaungwa mkono na Rais wa Marekani Donald Trump.
Urusi inasema mamlaka ya sasa ya Ukraine sio halali kwani Rais Volodymyr Zelensky amesalia madarakani hadi mwisho wa muhula wake na kwa hivyo sio mshirika halali wa mazungumzo.
Ikulu ya White House ilisisitiza kuwa utawala wa Ukraine utaamuliwa na katiba na watu wake. Matamshi ya Putin yanakuja wakati Marekani ikitaka kusuluhisha usitishaji mapigano katika vita ya Urusi na Ukraine, ambavyo sasa vimeendelea kwa mwaka wa nne.
Hata hivyo, siku ya Jumanne, Ikulu ya White House ilisema pande hizo mbili ziliweka makubaliano madogo ya kusitisha vita katika Bahari Nyeusi. Lakini Urusi iliweka mbele orodha ya masharti ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo vya nchi za Magharibi, na kusababisha wasiwasi kwamba Urusi ilikuwa inajaribu kuzuia hatua zozote za kusitisha mapigano.
Akizungumza na wanamaji wa nyambizi inayotumia nguvu za nyuklia katika mji wa Murmansk kaskazini mwa Urusi, Rais Putin alisema utawala wa muda Ukraine chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa unaweza kujadiliwa na Marekani, na nchi za Ulaya.