
Kampuni kubwa ya ubashiri Tanzania Meridianbet, imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kusaidia kwa vitendo. Kama ilivyo desturi yao kila mwezi, leo imefanya zoezi la ugawaji wa vyakula kwa wanawake wajane na wasiojiweza katika maeneo ya Magomeni.
Wanawake wajane mara nyingi wanakutana na changamoto kubwa za kiuchumi, hasa katika familia zinazozalisha mapato kidogo. Katika maeneo mengi kama Magomeni, wanawake hawa wanakosa msaada wa kifedha na kiutamaduni, na maisha yao yanaendelea kuwa magumu. Meridianbet imeona umuhimu wa kuchukua hatua katika kusaidia kundi hili la wanawake, ambao kwa mara nyingi hupuuziliwa mbali na jamii.
Kwa hiyo, Meridianbet imetoa msaada wa vyakula kama vile Unga, sukari, mchele, maharage, mafuta ya kupikia na bidhaa nyingine muhimu za nyumbani. Lengo ni kutoa msaada wa haraka ili kupunguza mzigo wa kifedha kwa wanawake hawa na familia zao, huku tukiwaonyesha kwamba wao si peke yao katika changamoto hizi.
Pia Jumamosi ya leo unaweza kuwa bingwa ambapo zaidi ya mamilioni kutolewa leo. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Keno, Poker, Roullette, Keno, na mingine kibao.

Wanufaika wa msaada huu walitoa shukrani zao kwa Meridianbet kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii. Bi Amina Mohamed, mmoja wa wanufaika wa msaada huo, alisema, “Tunashukuru sana Meridianbet kwa moyo wao wa upendo. Chakula ni kitu muhimu kwa kila mtu, na msaada huu umetufikia kwa wakati muafaka. Mungu awabariki sana na waendelee na moyo huu wa kusaidia.
Pia, Meridianbet inatambua umuhimu wa kuwa na ushirikiano wa karibu na jamii ili kuhakikisha msaada huu unafika kwa wale wanaohitaji zaidi. Kwa kushirikiana na viongozi wa kijamii na viongozi wa mitaa, tunahakikisha kuwa msaada huu unafika kwa wanawake wajane walioko kwenye hali ngumu, ambao wanahitaji msaada wa haraka ili kuboresha maisha yao ya kila siku.
Pamoja na kutoa msaada wa vyakula, Meridianbet pia inakusudia kuendelea na miradi mingine ya kijamii ambayo itakuwa na manufaa kwa jamii kwa ujumla. Tunajivunia kuwa na sehemu muhimu katika kuboresha maisha ya watu na kuleta mabadiliko chanya, kwa kuhakikisha kwamba tunajitolea kusaidia na kujenga jamii zenye ustawi zaidi.
