×

Leyla Akutana Na Baba’ake Baada Ya Miaka 3, Atokwa Machozi – Video

Leyla Shabani Mrosa (23), binti aliyepata ufaulu mkubwa na kufadhiliwa kusoma nchini India lakini baadaye kukatisha masomo kutokana na ugonjwa, hatimaye ameonana na baba yake mzazi ikiwa ni miaka mitatu tangu walipoonana kwa mara ya mwisho.

Leyla alikuwa akizungumza kwa simu tu na baba yake kwa miaka yote mitatu kutokana na sababu mbalimbali za kifamilia.

Akizungumza huku machozi yakimtoka, Leyla ameonesha jinsi anavyompenda baba yake.

Pia, baba yake ameonesha upendo wake kwa binti yake na kumuomba mama Leyla amruhusu aweze kumuona kila anapohitaji.

📞 Wasiliana na mama yake mzazi kwa msaada wowote:
📞 0679 282 278
📞 0756 809 334 (Nuru Jumbe)