×

Video: Familia ya Mzee Flavian Yaomba Rais Samia Kuwasaidia kurejeshewa ardhi yao Mbezi Beach, Dar

Familia ya Mzee Flavian Nyendikuu imemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuingilia kati na kuwasaidia kurejeshewa ardhi yao, ambayo wanadai kunyang’anywa na kupewa watu wengine, licha ya Mahakama kuamua kuwa ardhi hiyo ni mali ya Mzee Nyendikuu baada ya kushinda kesi ya mgogoro uliodumu kwa miaka 39.

Ardhi hiyo inahusisha viwanja namba 2107 na 2120, vilivyopo Mtaa wa Kilongawima, Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Baada ya Mahakama kutoa hukumu na kuthibitisha kuwa Mzee Nyendikuu ndiye mmiliki halali wa eneo hilo, familia yake ilianza mchakato wa kutafuta hati miliki kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Hata hivyo, walikumbana na changamoto kubwa katika mchakato huo.

Mwaka huu wa 2025, wamegundua kuwa viwanja hivyo tayari vimepewa hati kwa watu wengine, ambao wameanza ujenzi kwenye maeneo husika.

Hali hii imewasikitisha sana, na sasa wameamua kupeleka kilio chao kwa Rais Samia Suluhu Hassan, wakimuomba awasaidie ili wapate haki yao.