
Kuna hofu huenda Sudan Kusini ikatumbukia tena katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Uganda imetuma majeshi nchini humo kuunga mkono serikali ya Rais Kiir baada ya jeshi la Sudan Kusini wiki iliyopita kushambuliwa na wapiganaji ambao serikali imesema ni watiifu kwa makamu wa Rais Riek Machar ambaye sasa yuko kifungo cha nyumbani.
Ziara ya Rais Museveni inakuja siku moja tu baada ya wapatanishi wa Umoja wa Afrika kuwasili Juba kujaribu kuusuluhisha mzozo huo wa Sudan Kusini.
Mnamo mwaka 2018,Rais Kiir na Machar walitia saini makubaliano ya amani ya kuvimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu wa miaka mitano na kusababisha karibu theluthi moja ya idadi jumla ya watu wa taifa hilo kuachwa bila ya makazi na wengine wengi kuwa wakimbizi.