
KOCHA Mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema ambaye kwa sasa yupo kwenye benchi la ufundi la timu ya Wanaume Edna Lema amefichua alichoongea na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said.
Katika mchezo dhidi ya Coastal Union, uliochezwa Aprili 7 2025 ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza kukaa kwenye benchi la ufundi ambalo linaongozwa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Yanga ilikomba pointi tatu muhimu kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Pacome Zouzoua dakika ya 34 akitumia pasi ya Maxi Nzengeli aliyetumia mguu wa kulia kupiga pasi hiyo elekezi akiwa nje ya 18.

Mara baada ya mchezo, Edna alionekana akizungumza na Injinia Hersi ambaye alikuwepo Uwanja wa KMC Complex kwenye mchezo huo wa ligi mzunguko wa pili.
Edna amesema: “Unajua Rais Hersi ni mtu wa mpira na anafuatilia mengi yanayoendelea, mpira ulipoisha aliniuliza nimejifunza kitu gani na kuna nini ambacho nimekipata kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union.
“Ni mtu ambaye huwa tunazungumza naye masuala ya maendeleo ya mpira hivyo kuna mengi ambayo tumezunguma. Kukaa kwangu benchi ni furaha na ipo wazi kwamba kila hatua ni njema.”
Yanga kwenye msimamo wa ligi ni namba moja ikiwa na pointi 64 baada yakucheza mechi 24 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 62.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.