

Rais Samia Suluhu Hassan amewapongeza waandaaji wa Tuzo za Samia Kalamu Awards kutokana na tuzo hizo kuangazia pia eneo la Nishati Safi ambalo ni ajenda ya Tanzania Kimataifa na kusema kuwa amefurahi sana kuona waandishi wa Habari wanaandika kuhusiana na sekta hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutoa tuzo hizo, Rais Samia amesema, suala la Nishati safi ni ajenda ya Tanzania na kilichofanyika kwa wanahabari katika kukuza ajenda hiyo ni jambo ambalo linaonesha uzalendo mkubwa.
Amesema, ajenda ya Nishati Safi itasaidia utunzaji wa mazingina kwani takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya hekari laki 4 za misitu zinakatwa ili kupata nishati kwenye maeneo mbalimbali nchini.


