×

Mwanamitindo wa TikTok, Valeria Marquez, Auawa kwa Kupigwa Risasi Akiwa Live

 

Mwanadada Valeria Marquez

Mwanadada Valeria Marquez, mwenye umri wa miaka 23 na raia wa Mexico, ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa live kwenye mtandao wa TikTok, Jumanne, huko Mexico.

Tukio hilo limetokea katika mji wa Guadalajara, baada ya mtu mmoja kuingia katika saluni ya mwanadada huyo na kumpiga risasi.

Polisi mjini humo wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, ambalo linaelezwa kuwa ni muendelezo wa matukio ya mauaji dhidi ya mabinti na wanawake nchini humo.

 

Katika taarifa ya hivi karibuni, Umoja wa Mataifa ulieleza kuwa kila siku wanawake na mabinti 10 huuawa na wapenzi wao, ndugu, jamaa au marafiki.

Kabla ya kifo chake, Valeria alikuwa ameketi ndani ya saluni yake huku akiwa live kwenye TikTok. Sekunde chache baadaye, alishambuliwa kwa risasi hadi kufariki dunia.

Video hiyo ilisita ghafla baada ya mtu aliyekuwa karibu kuichukua simu na kuifunika kamera, ili kuficha yaliyokuwa yanaendelea baada ya tukio hilo.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa Valeria Marquez aliuawa na mtu aliyekuwa ameigiza kutaka kumpa zawadi.

Zaidi ya wafuasi 200,000 waliokuwa wakimfuatilia Valeria kwenye TikTok na Instagram wameonyesha masikitiko na hasira, wakilitaja tukio hilo kama kitendo cha kinyama.

HARMONIZE AVUNJA UKIMYA KUHUSU IBRAAH – “HUU NDIYO MSIMAMO WANGU RASMI”… – ATOA TAARIFA kwa UMMA..