×

Nyuma ya Pazia Kolabo za Mondi na Wakongo

UKWELI ni kwamba kuna siri kuu moja ya msanii wa Bongo Fleva nchini Diamond Platnumz kufanya kolabo na wanamuziki wa DR Congo kwani tayari amewashirkisha kwenye nyimbo zake tatu.

 

Novemba 25 mwaka huu msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz aliachia wimbo wake aliomshirikisha mkongwe wa muziki Afrika, kutokea DR Congo, Koffi Olomide, iliokwenda kwa jina la Waah!

 

Kolabo hiyo na mkali huyu wa muziki wa Soukus ilikuja siku chache mara baada ya Kofii kumtembelea Diamond nchini na mara moja wakaigia studio na kufanya jambo lao, lakini kwa nini Koffi Olomide?

Ukweli ni kwamba nyimbo ambazo Diamond amefanya na wasanii wa DR Congo zimekuwa na mafanikio makubwa Mke huyo wa Rapa Jay Z alifahamu kuwa nchini hiyo ina idadi ya watu zaidi ya milioni 200 wanaofahamu lugha ya Kingereza hivyo atapata mafanikio makubwa Zaidi kisoko kwa kuwashirikisha wasanii wa huko ukilinganisha na zile alizofanya na wasanii kutokea mataifa mengine kama Nigeria, Afrika Kusini, Kenya, Marekani n.k.

 

 

Kipimo ambacho kimekuwa kikitumiwa na wasanii wengi nchini kutoa ishara ya wimbo uliofanikiwa ni idadi ya waliotazama katika mtandao wa YouTube, ingawa njia hii imekuwa akikabiliana na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wasanii waliofanya Bongo Fleva toka miaka ya 2000 na kufanikiwa vilivyo.

 

Diamond ameamua kupima kolabo zake za kimataifa kwa kutumia njia hiyo ya You Tube. Kolabo alizofanya na Innoss’B na Fally Ipupa zimekuwa na mafanikio makubwa YouTube kuliko zile alizofanya na Davido, Mr. Flavour, Iyanya, Patoranking, P Square, Ne-Yo, Omario, Rick Ross n.k.

 

Video ya Wimbo wa Yope Remix alioshirikishwa na Innoss’B uliotoka Septemba 7, 2019 imetizamwa zaidi ya mara milioni 125 tangu itoke

 

imetizamwa katika Mtandao wa YouTube zaidi ya mara 100 milioni ikiwa ni video yake ya pili kutazamwa zaidi katika chaneli yake.


Kolabo hizi mbili alizofanya na wakali hawa kutokea DR Congo, ndani ya mwaka mmoja zimevunjilia mbali rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na “Nana’ kolabo aliyofanya na Mr. Flavour kutokea Nigeria miaka mitano iliyopita. Video ya wimbo “Nana” iliyotoka Mei 29, 2015 ndio ilikuwa inaongoza kwa kutizamwa zaidi ya mara 79 milioni.

 

Kutokana na mafanikio hayo, ndio maana Diamond amekuwa anajikita kufanya kolano na wasanii kutoka DR Congo ili kuendeleza moto wake huo aliyouwasha mwenyewe.

Lakini kwa nini wasanii wa DR Congo pekee ndio wanamleta mafanikio haya na sio mataifa mengine?

 

Kwa mujibu wa mtandao wa kutoa takwimu za papo hapo, Worldometers inakadiri nchi ya DR Congo kuwa idadi ya watu zaidi ya milioni 89.5. Watu wao wanazungumza Kifaransa kama lugha rasmi, pia kuna Kikongo (Kituba), Kilingala, KiTshiluba na Kiswahili, huku kukiwa na lugha zaidi ya 200 za makabila mbalimbali.

 

Lakini kifaransa pa kinazungumzwa na ni lugha rasmi katika nchi 29 duniani na wengi wao ni wanachama wa Organisation international De la Francophone, yaani jumuiya ya nchi 84 zinazotumia kifaransa kama lugha rasmi. Pia kifaransa ni moka ya lugha sita zinazotumika Umoja wa Mataifa (UN), hivyo kuwatumia wanamuziki wa DR Congo wanaochomekea kifaransa kwenye goma wanazofanya Kolabo na Diamond, kuna kitu kinaongezeka kwa mashabiki.

 

Kiswahili kutumika nchini DR Congo kunamuongezea pia Diamond uwanja wa kuuza muziki wake na ndio sababu ya kolabo anazofanya na wasanii kutokea nchini humo hufanya vizuri kwenye You Tube.

 

Hii ni faida kuliko anapofanya kazi wasanii kutoka nchi kama Nigeria na Marekani ambapo wanaofahamu Kiswahili ni wachache mno.

Sasa Diamond ikichukua idadi ya Watanzania wanaokadiriwa kufikia milioni 59, kwa mujibu wa Worldometers, na wale milioni 89 wa DR Congo ambapo idadi kubwa ya wanaotokea mataifa haya wanafahamu Kiswahili hufanya ngoma zake akifanyanao kolabo kutazamwa na watu wengi.

 

Mbinu hii ya pili, ndio aliyoitumia Beyonce kutokea Marekani kwa kuwajaza wasanii kama Tekno, Yemi Alade, Mr Eazi, Tiwa Savage, Wizkid na Burna Boy wote kutokea Nigeria katika albamu yake inayokwenda kwa jina la “Lion King”.

 

Mke huyo wa Rapa Jay Z alifahamu kuwa nchini hiyo ina idadi ya watu zaidi ya milioni 200 wanaofahamu lugha ya Kingereza hivyo atapata mafanikio makubwa zaidi kisoko kwa kuwashirikisha wasanii wa huko.

Leave a Comment