
Mmoja wa mwanafunzi wa kike akifanya wasilisho la mradi wa kundi lake kama sehemu ya kilele cha Wiki ya Ubunifu na Future Ready Summit jijini Dar es Salaam. Mradi huo ni sehemu ya programu ya ‘Code Like A Girl’ inayoendeshwa na taasisi ya dLab kwa udhamini wa Vodacom Tanzania PLC, ikilenga kuwajengea wasichana ujuzi wa TEHAMA na kuwahamasisha kupenda masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM).


