×

Uwoya: Sivutiwi na Wanaume Wenye Muonekano Mzuri

Irene Uwoya

STAR wa Bongo Movie mwenye mvuto wa pekee na mshiriki wa shindano la Ijumaa la Figa Bomba, Irene Uwoya, amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa havutiwi na wanaume wenye muonekano mzuri na hujui ni kwa nini

Ujumbe wa Irene Instagram

Aidha staa huyo amewahi kuripotiwa na vyombo vya habari kuwa anavutiwa sana na wasanii wa Bongo Fleva hasa wale wadogo kama Msami Baby.
“Kitu ambacho hamkijui kuhusu mimi ni kuwa SIJAWAHI kuvutiwa na wanaume wenye mionekano mizuri, sielewi ni kwa nini lakini wanaume wenye sura mbaya huwa wanaamsha hisia zangu za KIMAPENZI…’ aliandika Irene

 

salum Milong/GPL