×

Mbunge Shigongo Aeleza Hatari Ya Homa Ya Ini Nchini, Aomba Serikali Kuwachanja Watanzania – Video

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo ameitaka serikali kuchukua hatua zaidi za kudhibiti homa ya ini (Hepatitis B) ambayo kwa sasa inaathiri asilimia 6 ya Watanzania kwa kutoa chanjo kwa Watanzania.

Shigongo aliyasema hayo nje ya viwanja vya bunge baada ya kuchangia hoja katika Bajeti ya Wizara ya Afya iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma.