×

Sophy Juakali Aweka Wazi Mapenzi Yake ya Siri na Mume wa Mtu

Staa wa filamu Bongo, Sophy Juakali.

 

STAA wa filamu Bongo, Sophy Juakali, ametikisa mitandao baada ya kuweka wazi kuwa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mume wa mtu, akidai kuwa wanapendana sana na hana majuto yoyote kuhusu uhusiano huo.

Kupitia mahojiano yaliyosambaa kwa kasi mitandaoni, Sophy alifunguka bila woga akisema:

“Hivi mnajua kuwa mume wa mtu ni mtamu sana? Mimi sina mwanamme wangu pekee, nipo kwenye penzi na mume wa mtu. Nampenda sana na yeye ananipenda sana.”

Kauli hiyo imeibua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya mashabiki wakimshangaa kwa ujasiri wake, wengine wakimkosoa vikali kwa kuvunja misingi ya ndoa na maadili ya jamii.

Sophy, anayejulikana kwa uhusika wake mkali kwenye filamu za kibongo, ameonekana kutoyumbishwa na maneno ya watu, huku wengine wakidai huenda ni kiki ya kutafuta kiki au kujitengenezea headline mpya.