
Mhadhiri Msaidizi na Mtaalam wa lishe kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Kassim Mohammed Ally ameelezea jinsi ya kuimarisha afya kwa kutumia lishe bora kwa kuzingatia makundi ya vyakula pamoja na kufanya mazoezi.

Mhadhiri huyo amesema endapo utazingatia mlo kamili uliokamilika utaweza kuimarisha afya yako kwa kuepukana na maradhi mbalimbali kuwa kupata lishe bora.

Akizungumza na wanahabari wetu kwenye Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere vilivyopo Barabara ya Kilwa Jijini Dar Mhadhiri huyo amewataka wananchi kuzingatia lishe bora na kufanya mazoezi.

Akiyachambua makundi ya vyakula amesema kuna makundi sita ya vya kula ikiwemo wanga na protini ambavyo hupatikana kutoka kwenye mimea na wanyama. Alimaliza kusema Mhadhiri huyo.
HABARI/PICHA: NEEMA ADRIAN NA RICHARD BUKOS /GPL