
Staa wa muziki wa kizazi kipya kutoka Uganda, Bebe Cool, ametamka wazi kuwa Diamond Platnumz ndiye msanii namba moja bora Afrika Mashariki kwa sasa.
Bebe Cool, ambaye kwa sasa anatikisa anga la muziki na vibao vikali kutoka kwenye albam yake mpya “Break the Chain”, ametoa kauli hiyo usiku wa kuamkia leo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mbali na safari yake ya kimuziki, Bebe Cool amefichua kuwa yupo Tanzania kwa ajili ya kuitangaza rasmi albam hiyo, pamoja na kufanya mashirikiano ya muziki (collabo) na baadhi ya mastaa wa Bongo Fleva.