
INAELEZWA kuwa mabosi wa Yanga SC wamefanya mazungumzo na beki wa Yanga SC, Dickson Job kuhusu kuongeza kandarasi mpya kuendelea kuwa mali ya Wananchi.
Job alikuwa chaguo la kwanza msimu wa 2024/25. Wakati Yanga SC ikitwaa ubingwa wa ligi ya NBC na pointi 82 kwenye mechi 30 ambazo ni dakika 2,700 Job alicheza jumla ya mechi 26.
Ni mechi nne pekee alikosekana ndani ya msimu ambazo ni dakika 360 ndani ya uwanja. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Job alikuwa mfungaji wa bao la kwanza kwenye ligi ndani ya Yanga SC msimu wa 2024/25 umegota mwisho bila yeye kufunga.
Taarifa zinaeleza kuwa Yanga SC inahitaji kuendelea kupata huduma yake jambo ambalo limefanya mabosi wat imu hiyo kufanya naye mazungumzo.

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Yanga SC aliweka wazi kuwa kwa mchezaji ambaye wanahitaji huduma yake itakuwa ngumu kuodoka kwenye kikosi hicho.
“Ikiwa mchezaji tunahitaji huduma yake basi tutaweka hela ili abaki. Unakumbuka kuhusu Aziz Ki? Kuna timu zilikuwa zinamuhitaji lakini tukamuongezea mkataba.”