
Msanii wa filamu nchini, Lumole Matovolwa almaarufu Big au Kobisi Kikala, amefunguka kupitia Global TV na kufichua kuwa jina lake jipya la utambulisho, “Jobless wa Taifa”, lilitokana na ushauri wa mashabiki wake waliotaka atambulike kwa jina linaloendana na uhalisia wa maisha yake ya kisanii.
Kobisi amesema mashabiki wake walimshawishi kutumia jina hilo kutokana na namna wanavyohusiana na kazi zake, hususan majukumu anayoyabeba katika uigizaji, ambayo mara nyingi huakisi maisha ya kijamii.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.