×

Harmo Asepa na Kijiji Mbele ya Rayvanny

KABLA ya mambo kwenda mrama na kuwa maadui, wasanii wawili wa Bongo Fleva, Harmonize na Rayvanny walikuwa marafiki wakubwa ndani ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya Diamond Platnumz.

Lakini mara tu baada ya Harmonize au Harmo kusepa na kwenda kuanzisha lebo yake ya Konde Gang Music, kinachoendelea ni ubabe kati yao huku kila mmoja akitaka kuthibitisha ukubwa wake kwa mwenzake.

 

Baada ya Harmonize kuanzisha Konde Gang, Rayvanny naye akaanzisha Next Leve Music, lakini yeye akiendelea kuwa ndani ya WCB.

Baada ya Harmonize kujiita tembo, Rayvanny naye akajiita Chui.

 

UBABEUBABE TU

Baada ya Harmonize kujiita Teacher (Mwalimu), Rayvanny akajiita Lecturer (Mhadhiri) na ubabeubabe wa kimuziki unaendelea.

 

HARMONIZE ASEPA NA KIJIJI

Sasa; wikiendi iliyopita, Harmonize na Rayvany wakakutana kwenye jukwaa moja katika Viwanja vya Ngarenaro jijini Arusha na ndipo Harmo akasepa na kijiji mbele ya Rayvanny au Vanny Boy.

Aliyeanza kupanda stejini ni Rayvanny ambapo alipata shangwe kubwa na kila mtu kuamini kwamba yeye ndiye ameteka kijiji kwani watu walikuwa wakiimba naye nyimbo zake zote.

 

UWANJA WALIPUKA

Hata hivyo, baada ya Rayvanny ndipo akampisha Harmonize au uwanza mzima ulilipuka kwa kuita Jeshi…Jeshi…Jeshi…

Kilichofuata baada ya hapo ni Konde Boy kushusha shoo ya kihistoria akibebwa zaidi nay ale mangoma yake ya Amapiano ambayo yana vaibu kubwa ukilinganisha na nyimbo za Rayvanny ambazo nyingi ni za kuimbika kuliko kuchezeka.

 

Hadi mwisho wa tukio hilo, Harmonize akawa amethibitisha ukubwa wake mbele ya Rayvanny.

Uhasama wa Harmonize na Rayvanny ulikolea baada ya wawili hao kuwa kwenye uhusiano na mama na mtoto; yaani Harmonize na Kajala na Rayvanny na Paula ambapo zikawa zinavuja siri zao kiasi cha kufikishana Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar.

STORI; MWANDISHI WETU, ARUSHA

Leave a Comment