The House of Social Media
gunners X

Mnyika Awashauri Waliofungua Kesi Mahakamani Kuifuta – Video

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amewataka wale waliokishtaki chama hicho kuhusiana na uwepo wa mgawanyo wa rasilimaliza chama usio sawa, waiondoe kesi hiyo mahakamani ili chama kiweze kuendelea na shughuli za kisiasa ambazo sasa zimesimamishwa.

Akizungumza baada ya kuhudhuria na kusikiliza kesi hiyo iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Taifa Said Issa Mohamed na wengine wawili, Mnyika amesema: “Njia rahisi ya haraka sana ya kesi hii kumalizika ni wale walioshiriki kuitunga hii kesi kwa kuwatumia hao waliokuwa wajumbe wetu wa bodi kurudi kuiondoa hii kesi haraka sana turejee kwenye mapambano ya kisiasa bila vikwazo vyovyote”

Hata hivyo, Chedema katika kesi hiyo wamemkataa Jaji Hamidu Mwanga anayeisikiliza na Mnyika amesema miongoni mwa sababu zinazowafanya kumkataa jaji huyo ni kutokana na historia aliyonayo ya kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar lakini pia amri alizotoa mwezi uliopita kuhusu chama hicho.

Naye Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Rugemeleza Nshala amesema mahakama wamefafanua kuwa barua ya kutaka jaji ajitoe imepata leo, hivyo ombi hilo linatakiwa upande wa pili wapate nakala baada ya mawakili wao kusema hawajapata, hivyo jaji ameahirisha kesi hadi Julai 14 mwaka huu.
Mahakama imesema ni vema pande zote mbili zikasikilizwa hivyo siku hiyo anaweza kutoa majibu.

STORI NA ELVAN SITAMBULI | GPL

Comments are closed.